Mapigano ya Elimu dhidi ya Janga la Uviko 19

ByMartha Chimilila

Wadau wa Maendeleo katika nchi za Afrika Mashariki wanafanya kampeni mbalimbali za kuhakikisha watoto wanapata elimu bora na sio bora elimu. Katika kipindi cha mwaka 2020, dunia ilishuhudia mabadiliko makubwa haswa katika sekta ya elimu yaliyosababishwa na janga la Uviko 19. Mnamo mwezi machi 2020, nchi za Afrika Mashariki zilifunga Taasisi zote za elimu na hii ilitokana na muongozo uliotolewa na Shirika la Afya duniani ili kupunguza ongezeko la maambukizi ya ugonjwa wa Uviko 19.  

Baada ya miezi tisa, mnamo mwezi Januari 2021, Kenya ilifungua shule kwa wanafunzi milioni 16, licha ya wasiwasi wa wazazi. Vituo vya runinga vya Sauti ya Amerika na BBC viliripoti maelezo ya Waziri wa Elimu Kenya Bwana George Magoha akisema kuwa: 

“Napenda kuwasihi wazazi kuwaruhusu watoto warudi shule. Taratibu zote za kiafya tutahakikisha zinafatwa ili kuwalinda watoto dhidi ya janga hili” 

Nchini Uganda hivi karibuni Rais Museveni alitoa maamuzi ya kufungua shule mnamo Oktoba 2021. Bi. Janet Museveni, Waziri wa Elimu, alithibitisha kwamba;  

Kuendelea kufungwa kwa shule kunakusudiwa kulinda afya na maisha ya vijana ambao ni mustakabali wa Uganda” 

Msimamo wa serikali ya Raisi Museveni umezua ukosoaji kutoka kwa wapinzani nchini Uganda. Mmoja wa wapinzani nchini Uganda anayejulikana kwa jina la Dkt. Kizza Besigye katika moja ya mtandao wa kijamii aliandika msimamo wake juu ya kauli ya serikali ya Raisi Museveni na kuandika; 

“ Vijana 1000 wanakusanyika katika wilaya zote za Uganda ili kusajiliwa na jeshi la polisi kwa ajili ya mafunzo. Lakini Raisi Museveni anasema shule haziwezi kufunguliwa ijapokuwa amepata ushauri kutoka kwa wataalamu wake. Hiki ni kitendo cha usaliti kwa watoto wa kaya maskini nchini” 

“Uganda kufunga shule zetu kwa zaidi ya mwaka mmoja ni kosa kubwa. Hakuna haki yoyote kwa hatua ambazo zimechukuliwa dhidi ya shule. Tumejua watoto wameathiriwa kidogo na Uviko-19. Kwa nini ufunge shule na watoto kukosa maarifa sababu ya Uviko 19” 

Raisi Museveni alipata kujibu swali la Dkt Besigye siku ya maadhimisho ya Vijana duniani mnamo Agosti 12,2021.Alijibu kuwa; 

“Serikali inajua inachokifanya na haiitaji ushauri kutoka kwa mtu yoyote. Nilimsikia rafiki yangu Dk Besigye akiongea juu ya kufunguliwa kwa shule; kwamba shule zifunguliwe, Sawa asante sana Dkt Besigye, lakini haujapitia shida hiyo ipasavyo” 

Nchini Tanzania,hayati Raisi John Pombe Magufuli, aliishangaza dunia na watu wa Afrika Mashariki baada ya kuamuru kufunguliwa kwa shule mnamo mwezi Julai hii ni baada ya kufunga shule na taasisi za elimu kwa muda wa miezi mitatu. 

Julai mwaka 2021, mrithi wa Hayati Raisi Magufuli, Bi Samia Suluhu Hassan alitangaza jinsi Taasisi za elimu zinapaswa kuweka vifaa vya kunawa mikono. Miongozo mbalimbali imewekwa na serikali ya Tanzania katika harakati za kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa Uviko 19. 

Gazeti la Citizen la Julai liliripoti Prof Abel Makubi, katibu wa kudumu Wizara ya Afya Tanzania, kama aliamuru: 

 “Wizara ya Elimu inapaswa kuhakikisha shule na vyuo vikuu inaweka vipaumbele juu ya matumizi sahihi ya barakoa. Wanafunzi, walimu, wahadhiri wanapaswa kuvaa barakoa kila wakati. ” 

Mnamo Agosti 2021, Rwanda na Uganda walifunga tena Taasisi za masomo kwa muhula wa tatu kwa siku 15. Zuio hilo limekuja baada ya kuongezeka kwa iadadi ya maambukizi na vifo. Nchini Rwanda, taasisi za kujifunzia zilifungwa kwa miezi 10 kutoka Machi 2020 na kufunguliwa mnamo Novemba 2020. Takwimu za Benki ya Dunia zinasema hii ilifunga wanafunzi wasiopungua milioni 3.5. 

Kama ilivyo Kenya na Tanzania, Rwanda iliwaamuru wasimamizi wa shule, walimu, wanafunzi na wataalamu wa afya kufata miongozo ya afya kama kuvaa barakoa katika mikusanyiko ya watu, kunawa mikono na maji tiririka na kufungua madirisha. 

Source: https://www.thecitizen.co.tz/tanzania/news/east-africa-news/how-tanzania-rwanda-and-kenya-kept-schools-open-in-a-middle-of-covid-19-3555510 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *