Mapigano dhidi ya Minyororo ya Ulawiti, Rwanda

By Martha Chimilila

Ukatili wa kijinsia ni kitendo anachofanyiwa mtu yoyote kwa lengo la kumdhuru au kumuumiza kisaikolojia, kimwili, kiafya, kingono na kiuchumi. Tafiti nyingi zinaonyesha kuwa, wanawake ndiyo wahanga wakubwa wa ukatili wa kijinsia. Hali imekuwa ya tofauti nchini Rwanda, ambapo Wataalamu wametoa ripoti inayoonyesha asilimia 11 kwa mwaka wamefanyiwa ukatili wa kijinsia kwa watoto wa kiume(ulawiti). Ulawiti ni kitendo cha mtoto wa jinsi ya kiume kufanya ngono, kinyume na maumbile.

Taasisi ya makosa ya jinai nchini Rwanda, ilitoa ripoti mnamo Februari 2021. Ripoti hii inaonesha hali ya hatari kutokana na ongezeko kubwa la vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto wa kiume (vitendo vya ulawiti). Kwa mwaka 2019/20 ripoti imeeleza kuwa zaidi ya visa 111 ya vijana wa kiume waliofanyiwa vitendo vya ulawiti.

Baadhi ya waathirika wa vitendo hivi walieleza kuwa walipata, maaambukizi ya magonjwa sugu kama vile Ukimwi. Mmoja wa waathirika alitoa simulizi ifuatayo;

Nilitoka nyumbani mida ya jioni kwenda kuchota maji na nilipokua njiani nilikutana na mtu mmoja akaniomba kunisaidia kubeba maji. Baada ya dakika kadhaa nilimuona akichomoa kisu na kuniamuru kulala chini. Akasema nikipiga kelele atanichoma kisu, alinivua nguo na kunipaka mafuta katika sehemu ya kutolea haja kubwa na kufanya mambo yake. Siku hiyo niliumia sana na nilipofika nyumbani sikusema chochote

Idadi kubwa ya watoto waliofanyiwa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia huficha matatizo walioyapata, hii imetajwa kama sababu ya kuongezeka kwa uzito wa tatizo hilo nchini Rwanda. Wana saikolojia wanasema kuwa watu wa aina hii wapo katika hatari ya kuharibika kimaono, lakini bado wana nafasi ya kurejea katika Maisha ya Kawaida. Bi Getrude Nyirahabineza, mtoa ushauri nasaha kwa watu waliopata matatizo hayo alisema yafuatayo;

Mtu aliyefanyiwa vitendo hivi vya matumizi ya nguvu Maisha yake huharibika na wengi huonekana wenye upweke na kujiona hana thamani katika jamii. Sisi huwa tunazungumza nao na kuwashauri, tunawaambia na kuwakumbusha kwamba jamii bado inawapenda na kuwathamini. Wengi wa waathirika hua wanachuki kwa jamii yao

Bwana James Ndahayo kutoka kituo cha taifa cha malezi na makuzi kwa watoto alisema wazazi wana jukumu la awali Kuhakikisha usalama wa watoto wao.

Ni vizuri wazazi kufatilia makuzi ya watoto tena kwa umakini na ukaribu sana. Wazazi hawapaswi kumuamini kila mtu, hata msaidizi wa nyumbani. Ni vizuri Mzazi kufatilia kujua mahusiano ya mtoto na msaidizi wa nyumbani. Ni muhimu kujenga urafiki na watoto ili waweze kuzungumza kuhusu Maisha yao ya kila siku
Serikali nchini Rwanda, Imetengeneza sheria kali zinazotoa adhabu kwa watu wanaojihusisha na vitendo hivyo kama kifungo cha Maisha jela, Ijapokuwa vitendo hivyo bado vinaendelea kuongezeka.  Mwezi uliopita mahakama mjini Kigali ilitoa hukumu ya kifungo cha maisha kwa mwanaume mmoja baada ya kukutwa na hatia ya kuwalawiti watoto wa kiume 17 kwa nyakati tofauti.

Nini kifanyike kupunguza tatizo hili?

Ufatiliaji na utekelezaji wa sera pamoja na, utoaji wa elimu na vifaa tiba kwa waathirika wa ukatili wa kijinsia(ulawiti). Watoa msaada wenye sifa zinazohitajika, maabara nzuri kwa ajili ya vipimo, Wataalamu wa sheria na sehemu salama za kujifunza kwa waathirika katika jamii.

Kutengeneza sera rafiki itakayo toa maelezo ya wazi kuhusu viashiria vya mtu aliyefanyiwa vitendo vya ulawiti na nini kifanyike ili kuweza kuwasaidia wahanga wa vitendo hivi.

Ushirikiano baina ya wananchi, serikali na asasi za kiraia ili kuweza kupata taarifa sahihi na njia za kupunguza tatizo katika jamii.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *