Maneno Ambayo Hustahili Kumwambia Mwanao

By; Khadija Mbesa

Ulezi sio kazi rahisi, ila ni sehemu muhimu sana, ugumu wa uzazi ni kujifunza kuzungumza na mtoto wako, kwani Watoto huchukua kila kitu kihalisi na njia unayoongea nae huenda mbali katika kujenga utu wao.

Lakini kama mzazi yuko katika mauzauza huenda akamtupia ama kumrushia maneno ambayo hayapendezi kwa mtoto wake bila kusudia.

Kwa bahati mbaya, akili ya mtoto haijakuwa vya kutosha kuelewa kwamba maneno hayo hayakuwa yamekusudiwa na kwa sababu hiyo, huenda ikamlemaza akili.

Kutokana na Utafiti, jambo lililobakia ni kujifunza kupima maneno yanayotoka kinywani mwako kumwambia mwanao.

Kati ya yote, haya ni  kati mambo unayotakiwa kuzuia kumwambia mwanao.

  • Wewe si mtoto mwema; katu usimjaze mwanao na mawazo hasi kujihusu, kwani huenda akajishusha thamani, Bali muongeleshe kwa upole huku ukimwelezea makosa yake.
  • Mbona usiwe kama ndugu yako; Haya ni maneno ambayo Watoto wengi huambiwa, kisa na maana ndugu yake anafaulu kumshinda masomoni ama anamzidi na talanta flani, Watoto huhisi vibaya mno na wanahisi upweke sana.
  • Hutaweza kufanya; wewe kama mzazi usiwai fanya mwanao akose kujiamini, badala ya kumwambia hataweza, ni vizuri kumwambia ajaribu ama mufanye nyote.
  • Usinizungumzishe; Usiwai kata njia ya mahusiano baina yako na mtoto, kwani kuna mambo ambayo yanaweza kumkwaza mwanao na asiweze kukwambia.
  • Neno la, Mtoto wa kike au Mtoto wa Kiume hapaswi kufanya hivyo; Nini kilitokea na Usawa wa Kijinsia Jamani? Mtoto ni mtoto, wacha ajichagulie mwenyewe chenye anataka kufanya.
  • Acha baba aje, nitamwambia; Hili ni jambo la kawaida sana katika familia zetu za kiafrika, Mtoto akikosea, Badala ya kumkanya na kumuonyesha mwelekeo, wewe ndiye wa kwanza kumpatia vitisho vya kumsemea kwa babake. Hii husababisha wasiwasi na hofu kwa mwanao.
  • Hakuna atakayemtaka mtoto mbaya kama wewe; ‘Mtoto mwenye shida’ haijasababishwa na yeye peke yake, sivyo? Wazazi ndio wanapaswa kulaumiwa ikiwa watoto wanakuwa na shida. Malezi yako kama mzazi ndio yanamnoa mtoto wako.

La mwisho ni, usiwe na pupa ya kumlea mtoto wako kama vile ulililelewa na mzazi wako, Karne uliyoishi wewe ukiwa utotoni siyo karne atakayoishi mwanao. Kwa hivyo tujifunze kupima maneno yanayotoka vinywani mwetu tutakapokua tunaongea na Watoto wetu, Ama hata tutakapokua tunaongea mbele ya Watoto wetu. Kumbuka ukuaji na utu uzima ya mtoto wako inategemea na malezi yako kama mzazi.

follow us on

Twitter:https://twitter.com/mtotonews

subscribe to our YouTube channel:https://YouTube.com/mtotonewstv

Mtoto News is a Digital Online platform of news, information and resources that aims at making significant changes in the lives of children by making them visible. Read mtotonews.com or follow us on Twitter and Facebook@mtotonewsblog

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *