Makosa Afanye Mtoto, Adhabu Apewe Mzazi.

By Khadija Mbesa

Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Msemo huu umekita mizizi nchini China baada ya bunge la China kutoa maoni ya kuzingatia sheria ya kuwaadhibu wazazi ikiwa watoto wao wadogo wataonyesha “tabia mbaya sana” au watakapofanya uhalifu.

Katika rasimu ya sheria ya kukuza elimu ya familia, walezi wataadhibiwa na kuamriwa kupitia programu za mwongozo wa elimu ya familia ikiwa waendesha mashtaka watapata tabia mbaya au ya jinai kwa watoto walio chini ya uangalizi wao.

“Kuna sababu nyingi za vijana kufanya vitendo vibaya, na ukosefu wa elimu ya familia isiyofaa ndio sababu kuu,” alisema Zang Tiewei, msemaji wa Tume ya Maswala ya Bunge chini ya Bunge la Wananchi (NPC).

Rasimu ya sheria ya kukuza elimu ya familia, ambayo itakaguliwa katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya NPC wiki hii, pia inawahimiza wazazi kupanga wakati wa watoto wao wa kupumzika, kucheza, na kufanya mazoezi.

Katika miezi ya hivi karibuni, wizara ya elimu imepunguza masaa ya kucheza kwa watoto, ikiwaruhusu kucheza michezo ya mkondoni kwa saa moja Ijumaa, Jumamosi, na Jumapili tu.

Imepunguza pia kazi ya nyumbani na imepiga marufuku mafunzo ya baada ya shule kwa masomo makuu haswa mwishoni mwa wiki na likizo, ikijali mzigo mzito wa masomo kwa watoto waliozidiwa.

https://www.reuters.com/world/china/china-drafts-law-punish-parents-childrens-bad-behaviour-2021-10-18/

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *