By Martha Chimilila
Mimba za utotoni ni moja ya tatizo kubwa sana kwa miji mikubwa kama Dar es Salaam, nchini Tanzania. Wadau wa maendeleo na serikali ya Tanzania wanafanya kampeni mbalimbali za kupunguza tatizo la mimba za utoto na kuongeza idadi ya watoto wanaojiunga na Taasisi za elimu kwa shule za awali hadi sekondari.
kulingana na Gazeti la dijiti la Mwananchi la tarehe 30 Agosti 2021, kuhusu taarifa ya kupandishwa kizimbani, Kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la Raymond Dastan mwenye umri wa miaka 24. Raymond ni Mkazi wa kijiji cha Chamazi, wilaya ya Temeke. Kijana huyu alipandishwa kizimbani kwa kosa la kumbaka binti wa miaka 16, aliyekuwa anasoma shule ya sekondari Magonza.
Maelezo yaliyotolewa na Wakili wa serikali, Adv. Eric Shija ni kuwa, “Kati ya tarehe 18 Juni na 24 Julai, mwaka wa 2021 maeneo ya Chamazi, Raymond alimbaka binti wa shule ya sekondari, hali iliyopelekea kupata ujauzito na kusababisha kusimamishwa shule kwa binti huyo”
“Upelelezi wa kesi umekamilika, naiomba mahakama ipange tarehe ya kusoma mashtaka na kutoa hukumu inayostahili”
Hakimu Mkazi, Anna Mpesa alisema kuwa; “Dhamana ipo wazi, hivyo mshtakiwa anatakiwa awe na wadhamini wawili. Wadhamini hao wanapaswa kuwa na vitambulisho vya taifa na kila mdhamini atasaini bondi ya shillingi million 2”
Wakili Mpesa alihairisha shauri hilo hadi Septemba 13, 2021 ambapo shtaka litasomwa tena kwa mara ya pili. Kuna msemo wa Kiswahili unaosema “Tamaa mbele mauti nyuma”