Mabadiliko ya Teknolojia wakati wa Corona

By Martha Chimilila

Corona si janga la kwanza lililotokea Ulimwenguni, ila ni janga ambalo limeathiri kila kona ya dunia, hasa kwa watoto. Wananchi wengi wanakosa mahitaji muhimu kama huduma za afya, elimu na ulinzi sababu walizaliwa katika umaskini au ubaguzi wa rangi, kabila  au dini. Corona imeondoa pengo hilo la ukosefu wa usawa na athari za kijamii, kiuchumi na kiafya ambazo zinajitokeza na kutishia kuporomoka kwa haki za watoto.

Jamii, wanaharakati wa haki za Watoto, na wadau mbalimbali wakona muda fasaha wa kuandaa mpango Madhubuti wa kuwalinda Watoto wa kizazi hiki na kingine kwa kuwekeza katika afya na elimu, kujenga mifumo na huduma bora zinazoweza kuwafikia Watoto wote duniani.

Ili kuweza kusonga mbele kwa changamoto  ambazo zinawakabili Watoto ulimwenguni, ni muhimu kushirikiana katika kujenga kizazi chenye nguvu zaidi. Tutaweza kufanya hayo wakati tutatengeneza mipango Madhubuti itakayoendana na Mabadiliko ambayo yametokana na janga hili la Corona kwa Watoto wote ulimwenguni.

Janga la Corona limeleta uharaka wa matumizi ya teknolojia katika upande wa kujifunza. Dunia imeona umuhimu wake katika kipindi ambacho shule zilifungwa na teknolojia imechukua nafasi kubwa katika utoaji wa elimu mahali popote na wakati wowote. Sasa tunakabiliwa na fursa ya ‘mara moja-katika-kizazi’ kuunganisha kila mtoto aliye shuleni kwenye wavuti, na kutoa zana mpya, zinazoendeshwa na dijiti kuwasaidia kukuza ustadi wa kutambua uwezo wao.

Kutokana na Mabadiliko haya ya teknolojia zaidi ya nusu ya Watoto watategemea teknolojia kujifunza na kuendesha Maisha yao ya kila siku. Jamii inatukumbusha kutengeneza mipango Madhubuti ili Watoto waweze kupata elimu kwa njia ya mitandao na isiyo ya kimtandao. Ijapokuwa tafiti zinaonesha kuwa karibia asilimia 30 ya Watoto duniani hawakuweza kujifunza, hii ni kwa sababu ya ukosefu wa mitandao na umeme, lakini zaidi ya nusu ya watoto na vijana ulimwenguni wako upande mbaya wa mgawanyiko wa dijiti, wakipunguza ufikiaji wa fursa sawa na wenzao waliounganishwa.

Nini kifanyike ili kupunguza tatizo na kuleta usawa kwa Watoto ulimwenguni:

Kufanya tafakari za utoaji wa elimu kwa njia ya kidigitali ambapo itahusisha matumizi ya mitandao kama ujumbe mfupi ili kuweka usawa wa utoaji wa elimu. Kutengeneza mpango mikakati wa utoaji wa elimu kulinga na mazingira au ukanda husika. Utengenezaji wa zana za kidigitali utaleta Mabadiliko makubwa duniani katika dhima ya ufundishaji kwa Watoto. Kushirikiana na Mashirika mbalimbali ambayo yanafanya kazi kwa kutumia teknohama ili kukuza ubunifu wa kutengeneza mitahala mizuri ambayo itaweza kutumika duniani kote bila kuleta ubaguzi wa nchi au ukanda au kipato.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *