Kutekwa nyara na Kuuawa

By Khadija Mbesa

Hapo juzi tarehe 13 mwezi julai mwaka wa 2021, kulikamatwa mshukiwa aliyehusika na kutoweka kwa wavulana wawili huko Biafra, ndani ya eneo la Eastleigh katika Kaunti ya Nairobi.

Ndani ya masaa kadhaa ya kukamatwa kwake, mshukiwa huyo aliandamana na DCI kutoka Ofisi ya Utafiti wa Uhalifu na Ujasusi hadi mahali ambapo alidai kwamba ametupa miili ya wavulana wawili wenye umri wa miaka 12 na 13 kwenye kichaka karibu na Shule ya Serikali ya Kenya Kabete.

Moja ya miili ilitambuliwa na familia ya mtoto aliyepotea, katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Jiji, Junior Mutuku Musyoka mwenye miaka 12 alipotea tarehe 30 juni, aliuliwa baada ya wazazi wake kuitishwa fidia ya elfu hamsini za Kenya.

Baada ya masaa kadhi katika kusaka, mwili mwingine ulipatikana sehemu zizo hizo.

Mshukiwa huyo alikamatwa baada ya maafisa kumnyemelea anamoishi , huko kitengela kaunti ya Kajiado.

Muuaji huyo aliye na miaka ishirini Lakini, amekiri mauaji ya kinyama ya angalau vijana 13 tangu mwaka wa 2016. Alisema kwamba hakuwa anafanya mauaji hayo akiwa pekeyake bali alikuwa anasaidiana na mwenzake.

Junior Mutuku Musyoka ni mtoto mmoja kati ya watoto kumi waliopitia unyama huo huo mkononi mwa muuaji Masten Milimo Wanjala.

Watoto hawa ambao wanatoweka hafla, wanateswa, kutopewa chakula na mteka nyara hadi mwisho kuuliwa kwa sababu ya kukosekana pesa za kulipa fidia. Maafisa wako wapi wakati vitendo hivi vinatokea?. Wanaosimamisha haki kwa watoto na kwa binadamu wote wako wapi?

Hawa ni watoto ambao walikuwa wanapendwa na wazazi wao na wanaojaliwa mema, wamekatizwa maisha yao kwa sababu ya mnyonya damu asiye na huruma. Vilio vya wazazi hao vinaskika kila kona lakini hakuna lingine linaloeza fanywa ila kupata haki.

Tunawapa pole wazazi wote ambao wamepoteza maisha ya watoto wao mikononi mwa muuaji huyu ambaye amekua akifanya uasi huu mfululizo

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *