By Khadija Mbesa
Shirika la Save the Children linaita mwito wa kusitishwa kwa vita mara moja, kwani watoto 58 huko Gaza na watoto wawili kusini mwa Israeli wameuawa ndani ya wiki iliyopita tu. Zaidi ya watu elfu moja huko Gaza, pamoja na watoto 366 pia wamekuwa wahasiriwa wa majeruhi. Watoto karibia watatu wanajeruhiwa ndani ya kila lisaa limoja huko Gaza kwanzia mei tarehe 14 kwa sababu ya vita kati ya Israel na palestini. Makumi ya waisraeli pia walijeruhiwa.
Huduma za kuokoa maisha zinaelekea kuvunjika kwani laini za umeme zimeharibiwa katika mabomu hayo. Ugavi wa mafuta, ambao ni vyanzo pekee vya nguvu na umeme katika Ukanda wa Gaza ni mdogo sana, na Israeli imefunga mpaka ambao huingiza mafuta.
Karibia watoto 60 wameuawa huko Gaza ndani ya wiki moja. Je! Ni familia ngapi zaidi zinahitaji kupoteza wapendwa wao kabla ya jamii ya kimataifa kuchukua hatua? Je! Watoto wanaweza kukimbilia wapi wakati mashambulio ya angani yanayonyesha kwenye nyumba zao? Familia za Gaza wako katika hatua ya kuvunjika matumaini – wanaishi kuzimu bila mahali pa kukimbilia, hawana pa kulilia.
Maisha ya watoto hao yanakatizwa kabla ya kuona nuru ya maisha ya baadae, ndoto zao zinakatwa kinyama na kuwaacha bila matumaini ya kuona jua la siku ya pili.