Kukatwa Ndimi na Fidia

By Khadija Mbesa

Mwakilishi wa Wanawake wa Nakuru Lisa Chelule amewaarifu wazazi, machifu na wazee wa vijiji ambao walifunga kesi za unajisi katika Korti za Kangaroo baada ya kupokea fidia ili kutowaripoti wanyanyasaji hao kwa maafisa wa polisi.

Bi Chelule alisema kuwa ripoti hii ililetwa kwake ikiwa wazazi wengine walifungwa vinywa kwa kiasi kidogo cha Sh10, 000 tu, Mifugo au hata pia mifuko ya mtama ili wamalize kesi bila ya kuchukuliwa hatua.

Mwakilishi huyo wa Wanawake alisema, anajitahidi kuweza kuja na suluhu ya wahalifu hao ambao wanaficha uhalifu wao kwa fidia kidogo ili waepuke sheria, huku akifanya kazi kwa karibu na maafisa wa polisi, taasisi za kidini na Mashirika ya Jumuiya ili kuwapa nidhamu hasa wahasiri hao.

“Tutaenda kwenye vijiji ambavyo watu hufanya mipango ya ndani kwa ndani na tutamkamata mtu yeyote, pamoja na wazazi, wanaohusika katika mikataba hii ya chumba cha nyuma wakati wanaathiri maisha ya baadaye ya watoto wao. Wasichana hawa bado wako chini ya umri, kwa hivyo hatuwezi kuzungumza kuhusu fidia wala idhini kwani hilo ni unajisi. Hili ni swali la unyanyasaji wa kijinsia, ambalo linafanya kuwa tishio la usalama, ”Bi Chelule alisema.

Akiongea wakati akitoa hundi za bursary zenye thamani ya Sh9 milioni kwa wanafunzi 900 wenye uhitaji kutoka kaunti kumi na moja, ndogo, Chelule alisema kuwa alifurahishwa jinsi maafisa wa kutekeleza sheria hawajatulia na bado wanawafwatilia washukiwa wanaoaminiwa kuwapa ujauzito watoto wadogo.

“Tumejitolea kuangalia kiwango ambacho wasichana wanaacha shule. Maafisa wa elimu, machifu na maafisa wa kutekeleza sheria wamepewa jukumu la kuhakikisha kuwa, wasichana wanahifadhiwa shuleni. Ni sera ya serikali kwamba, wale ambao tayari ni wajawazito au wameathiriwa kwa njia yoyote wanapewa ushauri ili waweze kupata ujasiri wa kuanza masomo baada ya kujifungua, ”aliongeza.

Mnamo Februari mwaka huu, Gavana wa Nakuru Lee Kinyanjui alitaja Molo, Kuresoi Kusini na Kuresoi Kaskazini kuwa na idadi kubwa zaidi ya visa vya unajisi.

“Mikoa hii inarekodi kiwango cha juu zaidi cha watoto wanaoacha shule ,hii ikiwa ni wasichana wenye umri kati ya miaka 12 na 17 kutokana na ujauzito. Hili lazima likome! halikubaliki Kamwe, na natoa wito kwa machifu na wazee wa vijiji kuwa mstari wa mbele katika kuwatambua wahalifu ili waweze kukabiliwa na sheria. Baadhi ya wachafu hawa wanatembea huru baada ya kuharibu maisha na elimu ya wasichana wadogo. Azimio la kupambana na hatari hii haipaswi kupoteza mvuke, “gavana alikuwa amesema.

Bi Chelule alisema kuwa uchunguzi ulibaini kuwa wachafu waliwashawishi watoto wadogo na Mandazi, Kangumus, soda na taulo za usafi kabla ya kuwanyanyasa kingono.

Alimhimiza Katibu wa Baraza la Mawaziri la Elimu Profesa George Magoha, kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wa shule za msingi na sekondari wanapata taulo za kutosha za usafi.

“Hatutakubali mazoea ya kitamaduni yaliyopitwa na wakati ikiwa ni pamoja na ukeketaji na ndoa za mapema. Wazazi wanaopuuza majukumu yao hawatastahimiliwa katu. Tumeacha kufwatilia kile watoto wetu wanafanya hili likichochea tabia za kutowajibika.

Ukeketaji umekuwa ukichangia hali hii ya kusikitisha kwani wasichana wanahisi wanastahili kuolewa baada ya kufanya ibada hiyo. Wakuu wako chini ya maagizo makali ya kukamata wazazi au wazee wowote ambao wanadhibitisha ndoa za mapema, ”alionya mwakilishi huyo wa wanawake.

Mwaka jana, visa 52 vya mimba za utotoni viliripotiwa huko Kuresoi Kaskazini huku Bi Chelule akidokeza kwamba shule katika eneo lililoathiriwa ziwe na vifaa vya bweni kwa wasichana kama njia ya kupunguza hatari hiyo.

Wizara ya Elimu, tangu wakati huo imetishia kuwatia nguvuni wazazi ambao watoto wao wa kike walio chini ya umri wa miaka wanapata mimba na wanashindwa kuripoti waliohusika kwa maafisa wa polisi.

Wizara hiyo pia ilionya kwamba wazazi ambao wataingia katika mipango ya kijamii na wahalifu ili kukwepa sheria watakamatwa.

Source:https://www.kenyanews.go.ke/parents-chiefs-warned-against-settling-defilement-cases-in-kangaroo-courts/

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *