By Khadija Mbesa
Vita hutokea, Ugomvi hutendeka, lakini ni nini hutokea kwa watoto baada ya vinyang’anyiro hivyo vya kutaka kuibuka mshindi na mwenye nguvu zaidi?.
Migogoro husababisha mafadhaiko yenye sumu na shida za kiafya utotoni na hata ukubwani.

“Psychological Trauma”. Baada ya vita, Watu wengine wana tabia ya kuzingatia tu majeraha ya nje, bila ya kutambua kuwa saikologia yaweza kuvurugika, ya watoto ambao wazazi wao ama mji wao umeathiriwa na vita hivyo.
Watoto walio katika vita vibaya, mara nyingi wananyimwa mahitaji ya kimsingi, mazingira ya kusaidia kisaikolojia, fursa za elimu, ufundi, na rasilimali zingine ambazo zinakuza maendeleo mazuri ya kisaikolojia na afya ya akili.
Nakala hii inaelezea changamoto za afya ya akili zinazokabiliwa na watoto na vijana walioathiriwa na mizozo, hatua iliyoundwa kuzuia au kuboresha athari za kisaikolojia za uzoefu, hususan unaohusiana na mizozo.
Kunakadiriwa kuwa, zaidi ya watoto bilioni bado wanaishi katika mazingira ya vita na mizozo, na watoto hawa wanaendelea kuwa katika hatari zaidi, huku wakihitaji msaada kutoka pande zote za dunia.
Mzigo huu wa shida ya akili ambayo huchangiwa moto hasa kwa sababu ya unyonyaji na unyanyasaji wa Watoto.
Watoto wanaweza kupata PTSD sumbufu, kutoweza kulala na kuwa na unyonge na huzuni kila wakati.
Mabadiliko ya mazingira ya mtoto baada ya vita pia huchochea katika kiwewe cha saikolojia ya mwana. Kwa mfano tuseme vita vimetokea, na kwa vita lazima kuna watu watakaokata uhai wao, na kati ya hao walioaga dunia kuna watu ambao wameacha watoto wao majumbani mwao, Maisha ya watoto hao yatakatizwa pia, iwapo watu waliokuwa wanawategemea wametekwa na vita au mizozo. Hili likikusudia watoto kutoenda shule tena kwa ukosefu wa fedha na kutopata lishe bora kwa kutoweza kumudu mahitaji yao. Hili litafanya saikolojia ya mtoto kuwa na bughdha.
Kiwewe cha saikolojia yadhuru Maisha ya baadae ya mtoto.https://www.youtube.com/embed/8HWYLStBwPA?version=3&rel=1&showsearch=0&showinfo=1&iv_load_policy=1&fs=1&hl=en&autohide=2&wmode=transparent
Badala ya watu kukazana ili kuweza kusaidia watoto na watu walioathirika na vita, kwa nini tusijizatiti ili kuhakikisha vita hivyo havitatokea?. Kwa sababu iwapo vita vitatokea basi watoto ndio watakua katika hatari kubwa zaidi. Kazi za utotoni, Unyanyasaji, Unyonyaji, kiwewe cha saikolojia na hata kupoteza wazazi na walezi wao.
Huzuni, hasira, kujilaumu, kutoamini, unyogovu, na wasiwasi zote zimeandikwa vizuri kwa watoto ambao wamepata vurugu. Athari hizi zinaweza kuendelea hadi wakawa watu wazima.
Hata hivyo kuna changamoto nyingi zaidi zinazochochea kiwewe cha saikolojia ya mtoto lakini vita vimeshika mstari wa mbele.https://www.youtube.com/embed/WYriqfcIPpM?version=3&rel=1&showsearch=0&showinfo=1&iv_load_policy=1&fs=1&hl=en&autohide=2&wmode=transparent
Watoto hawa wanaendelea maisha yao wakiwa waathiriwa vita, zawadi za vita kwao ni kiwewe cha saikolojia hasa PTSD, unyogovu na hata kukosa matumaini ya jambo lolote. Dunia imewafelisha.
Tukomeshe Vita!. Athari za baada ya vita ni nzito mno. Tuwalinde wana wetu kutokana na Vita, Unyanyasaji na Unyonyaji.