Kiu ya Masomo na Karatasi za Hedhi

By Khadija Mbesa

Kuvunjika kwa mwiko si mwisho wa kupika Ugali, Watoto wengi wa kike walioweza kupata ujauzito wa mapema bado wana kiu ya kutaka kuendelea na masomo, na upande wa kinangoni wanafunzi wa kike wanatumia matambara wakati wa hedhi kwa kutoweza kumudu bei ya sodo.

Watoto wengi wa kike wanahadawa kwa kupewa vishilingi viwili na wanaume walipo na umri wa juu ili waweze kulala na wao kukisababisha kwao kupata mimba za mapema na kukosa mwelekeo wa Maisha. Watoto hawa wengi wana matumaini ya kuweza kurudi shuleni na kuendelea na masomo yao.

Uchambuzi unaoyesha kuwa, Zaidi ya Watoto elfu kumi wameweza kuwa wahasiriwa wa ujauzito wa mapema, hali ambayo nambari za wahasiriwa zinaendelea kuongezeka kila mwaka. Hili ni jambo la kusikitisha mno kwani Watoto hao wa kike wanakatiziwa ndoto zao kwa mapema.

Tukielekea upande wa pwani kinangoni, Watoto wa kike wametoa malalamishi ya kuwa, hawana uwezo wa kumudu bei ya sodo ikiwaelekeza wao kutumia matambara. Hali ambayo inaskitisha mno kwani matambara hayo yanaweza kuacha madoa ya hedhi kwenye nguo zao.

Suala langu la leo ni? mshangao kwa serikali kwani, badala ya kutolewa kondomu za bure, kwa nini wasiweze kutoa sodo ambazo zinaweza kutumika tena na tena

Hali hiyo ya kutolewa sodo za bure ambazo zinaweza kutumika tena, itasaidia sana kutokuwa na mimba za mapema za watoto wa kike, na pia upungufu wa dhulma ya kijinsia, kwani baada ya madoa hayo ya hedhi kuingia kwa nguo za shule za wanafunzi hao wa kike, wanafunzi wengi wa kiume huwacheka na kuwanyanyasa kijinsia kukiwasababishia wanafunzi hao wa kike kuwa na unyonge mno.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *