By Khadija Mbesa
Chanjo kwa watoto wa shule inaweza kuanza hivi karibuni, baada ya wizara ya afya kusema kwamba, bado inakagua data ya usalama juu ya chanjo hiyo, kati ya watu wenye umri wa kati ya miaka 16 na 18.
Mwenyekiti wa kikosi wa kazi ya kusambaza chanjo Dkt Willis Akhwale, alisema hapo Jumanne kwamba,jopokazi hilo, pamoja na ushirikiano wa kamati zingine za kiufundi za Wizara ya Afya wataweza kufanya uamuzi sawa katika wiki zijazo.
“Tunaangalia data katika matumizi ya Pfizer kwa watoto walio chini ya miaka 18, ambayo ni miaka 16 hadi 18 na katika wiki ijayo tutafanya uamuzi ambao una uwezekano mkubwa wa kuanza kuwachanja kwa kuwa tuna kipimo cha kutosha cha Pfizer,” Akhwale alisema.
“Wiki iliyopita tulipokea milioni moja ya dozi, na tutakuwa tukipokea karibia dozi nyingine milioni 3.7 za Pfizer kabla ya mwisho wa mwaka,” aliongeza.
Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) kinapendekeza kwamba, kila mtu mwenye umri wa miaka mitano na zaidi apate chanjo ya Covid-19 ili kweza kusaidia kujikinga dhidi ya ugonjwa huo.
Ingawa watoto wako katika hatari ndogo ya kuwa waathiriwa zaidi wa Covid-19 kuliko watu wazima, chanjo hii itasaidia kulinda familia nzima na kupunguza kasi ya kuenea kwa virusi katika jamii.
Data kutoka kwa tafiti za chanjo ya Pfizer zinaonyesha kwamba, chanjo hiyo ni salama na ni nzuri kwa watu wenye umri wa miaka 5.