By Khadija Mbesa
Ujana, Ngono na Utalii ni mambo ambayo yanaenda sambamba na yanapewa kipaumbele ndani ya roho ya Pwani Kenya. Mambo haya hayazingatii umri wala jinsia, watu wazima na hata Watoto wadogo wanaweza jipata ndani ya kisima hichi cha ukahaba.
Mzazi kumfundisha mwanawe jinsi ya kujiuza na kupata fedha kupitia kufanya mapenzi na watalii ni jambo la kawaida sana pwani, bila ya mzazi huyo kuzingatia hatari atakazopitia mtoto huyo. Kuzidi kwa umaskini kunawaendelezea waschana wa kike na hata wa kiume kuacha shule na kujiingiza katika dunia ya ukahaba na starehe, si hayo tu kwani baada ya kujiingiza katika silisili hiyo Watoto hao wataanza kua walevi wa mihadarati na Maisha yao huwa katika hatari Zaidi.
Maambukizi ya magonjwa ya VVU na Ukimwi, mimba za mapema na hata vifo vya mapema ni moja wapo ya mambo yatakayowakumba Watoto hao. Je ni mambo gani yanayoweza kuzingatiwa ili kupunguza maambukizi haya ya maradhi yasiyokuwa na tiba ya Ukahaba? Katika tamaa hii ya Kutaka pesa za haraka wazazi hawa wanatumbukiza Watoto wao kwenye shimo la giza lisilokua na matumaini ya mwanga.
Kati kati ya miti ya mitende kule pwani kuna msichana mdogo aliyekosa mwelekeo wa Maisha kwa sababu ya kujiingiza katika ukahaba. Licha ya sheria ya Kenya kusema kuwa idhini ya kufanya mapenzi kwa mtoto ni kwanzia miaka kumi na nane kwenda juu, na chini ya hapo itachukuliwa kama ubakaji na hukumu yake ni miaka ishirini ndani ya jela, wakaazi wengi wa Pwani ni kama wameweka maneno hayo nyuma ya visogo vyao.
Mabadiliko yanaanza na mimi Pamoja na wewe. Tukataze ubakaji na ukahaba wa Watoto!