Juhudi za Kukoleza Masomo kwa Watoto

By Martha Chimilila

Takribani asilimia tisa ya wazazi wanasoma vitabu vya hadithi pamoja na watoto wao, tafiti iliyofanyiwa na asasi ya kiraia (Save the Children), inasema kuwa asilimia tatu ya watoto wamekwishasoma vitabu vya hadithi kwa lugha ya Kinyarwanda. Serikali ikishirikiana na Mashirika mengine katika Mpango wa Maendeleo walianzisha kampeni iliyolenga kukuza kusoma vitabu au hadithi kwa watoto nchini Rwanda, asilimia 75 ya wazazi walioshiriki katika kampeni hii, walisema kuwa uhaba wa vitabu vya hadithi za watoto ndiyo changamoto inayowasumbua. 

Bi Perpétue Uwera, Mkurugenzi wa Shirika la Wachapishaji linalojulikana kwa jina la Perdue, lililopo mjini Kigali, alisema kuwa wachapishaji wanapaswa kupunguza gharama za uchapishaji wa vitabu ili kuongeza upatikanaji. Bi Uwera, aliongea na gazeti la The New Times na kusema yafuatayo; “watoto wengi katika maeneo ya vijijini hawana huduma ya kusoma vitabu kwa njia ya dijiti, ndiyo wana vitabu lakini vimekwama katika mkataba zao za shule” 

Pia, Bi Uwera alipendekeza uwepo wa maktaba za dijiti ili kuweza kupunguza tatizo la watoto kushindwa kusoma vitabu. Ijapokuwa anafahamu kuwa kutokana na janga la Corona (Uviko) itakuwa ni vigumu kutekeleza pendekezo lake la ‘vitabu vinaweza kupelekwa nyumbani, watoto wakasoma na kuvirudisha’ 

Bi Uwera, aliongeza kwa kupendekeza kuwa nyumba za uchapishaji zianze kutumia vitabu bure vya dijiti, kutumia redio ya jamii ambayo ni rahisi na vitabu vya sauti kwa watoto.  

Bi Betty Mukashema, Mwalimu wa Mary complex, alisema kuwa wazazi wanapaswa kuongeza juhudi za kusoma na watoto wao. “Wazazi wanapaswa kukuza utamaduni wa kusoma na watoto wao” 

Wakati shule zinapofunguliwa, walimu tunaona kupungua kwa uwezo wa kusoma sababu watoto hawakuwa wakisoma wakati wa likizo. Wazazi washiriki na watoto katika kusoma sio masomo ya shule bali hata vitabu vya hadithi mbalimbali za watoto” 

“Tutumie mitandao kuweza kupata vitabu vya hadithi. Wazazi tujitahidi kutengeneza tamaduni ya kusoma na watoto, tamaduni hii itawasaidia siku zijazo”  

Mwandishi Félicien Imanirafasha, ameeleza kuhusu kuzorota kwa tamaduni ya kusoma kwa watoto na kuongezeka kwa matumizi ya mitandao ya kijamii, ambapo watoto hutumia muda mwingi katika kutuma ujumbe mfupi, kuchapisha picha na kutazama picha zisizo na maadili. Aliongeza kwa kusema kuwa; 

Kwa kupitia vipindi vilivyosimamiwa, watoto wanaweza kuzingatia kusoma, wazazi wanapaswa kuhamasisha na kutenga muda mwingi wa kusoma kama muda unaotumika katika mitandao ya kijamii, lakini pia kuwanunulia vitabu. Ikiwa kila Kaya itatenga pesa ya kununua vitabu vya watoto kama wafanyavyo katika kununua vifaa vingine nyumbani. Hii itasaidia katika kujenga tamaduni ya kusoma vitabu kama sehemu ya elimu kwa watoto, basi tamaduni hii itakuwa na kuboresha mazingira ya familia zao kwa siku zijazo” 

Source: https://www.newtimes.co.rw/news/what-should-be-done-make-children-read-more 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *