Je ni Mila Ama Utumwa?

By; Khadija Mbesa

Tumejifanya viziwi na vipofu mbele ya mambo ambayo yanamdumisha na kumdhalilisha mtoto kwa kusingizia mila. Je mila hiyo haina huruma mbele ya Watoto? Si ukeketaji, si ndoa za mapema kwa wasichana, si kutosomeshwa, yote hayo yanamkosema mtoto wa kike fursa ya kuishi kwa furaha.

Ukeketaji

Si leo wala si kesho, tabia hii ya kukeketwa ilianza tangu jadi, wanavijiji wakisingizia ni mila zao ili wasichana wao waweze kuwa tohara, huku ni kuwakandamiza Watoto wa kike tu, kwani si uchungu tu bali watapata shida wakati wa kujifungua, na kuna uwezekano mkubwa kuwa wanaweza kupoteza Maisha yao wakati wa kujifungua.

ukeketaji ni ukiukaji wa haki za binadamu lakini unaathiri afya kimwili na kiakili kwa mamilioni ya wasichana na wanawake na pia kutumia raslimali nyingi muhimu za nchi na kwamba uwekezaji zaidi unahitajika kumaliza ukeketaji na madhila unaosababisha.

Ndoa Za Mapema

Huu ni ugonjwa ambao unawakumba sana dada zetu wa pwani, Garissa, Samburu n.k. Watoto wa kike wanalazimishwa kuolewa mapema kwa midai ya ‘waweze kusitirika’ hili si jabo geni kabisaa, na kinachosikitisha ni kwamba watu wameweka mazoea sana katika suala hili hadi mtoto mdogo wa kike akiolewa haiwi mshangao kabisaa.

Unaweza pata Watoto wengine wa kike wanakimbilia ndoa za mapema ili kukwepa shida za maskani mwao. Huku wakitupilia shule mbali.

Kutosomeshwa

Katika vijiji vyetu, Watoto wengi wa kike hawasomeshwi. Unaweza pata mzazi wa kike anataka kumwandikisha mtoto wa kike shuleni ili aweze kupata elimu, lakini mzazi wa kiume anakataa kabisa kujishirikisha na mambo hayo huku akisema yakwamba mtoto wa kike hafai kusomeshwa anafaa kuolewa.

Unaweza pata kuna kesi nyingi katika vijiji , mzazi wa kike kwenda kumshitaki mzazi wa kiume, katika kituo cha polisi ama hata kwa chifu wa mtaa kwa sababu ya kukataa kulipa sera ya mwanafunzi wa kike ama kukataa mtoto wake wa kike kupata fursa ya kusoma. Hii ni kupiga hatua moja mbele. Tusikubali kabisa mtoto wa kike kulazimishwa kukata masomo yake kwa madai ya MILA. Kwani mila hiyo kazi yake ni kumkandamiza mtoto wa kike tu? Tusiwe watumwa mbele ya mila zetu. Mila isiwe chanzo cha kuharibu Maisha ya mtoto yeyote, kila mtoto ana haki ya kusoma, ana haki ya kutoa maono yake, na ana haki ya kukataa kudhulumiwa.

follow us on

Twitter:https://twitter.com/mtotonews

subscribe to our YouTube channel:https://YouTube.com/mtotonewstv

Mtoto News is a Digital Online platform of news, information and resources that aims at making significant changes in the lives of children by making them visible. Read mtotonews.com or follow us on Twitter and Facebook@mtotonewsblog

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *