By Khadija Mbesa
Zaidi ya asilimia 80 ya watoto wanaoishi katika nyumba za utunzaji bado wana wazazi.
Baraza la Mafundisho ya Dini la Pwani linaongoza kampeni inayolenga kuwaunganisha tena watoto na familia zao.
Mpango huo ulioanzisha huko Kilifi katika kaunti ndogo ya Malindi, Magarini na Ganze Inahakikisha kuwa watoto hao wanalelewa kati kati ya jamii badala ya nyumba za watoto.
Kufikia sasa, mpango wa uhamasishaji unaendelea kwa kiwango kikubwa ambapo machifu wanafunzwa jinsi ya kusaidia watoto wakati wa mchakato wa ujumuishaji.
Mpango huo unahakikisha watoto wanaweza kupata usaidizi kutoka kwa taasisi za misaada.
Hili si suala geni ambapo mzazi anatoweka kwenye maisha ya mtoto wake, au kupoteleana kwa mzazi na mwanawe. Ila mpango huu wa kutowapeleka watoto kwenye nyumba za utunzaji wa watoto bali kuwalea katika jamii inawasaidia sana watoto hawa na kuwakuza wakiwa na maadili na ustarabu wa kijamii.
Kisa kilichowalizimisha watoto hawa kupelekwa kwa nyumba za utunzaji na wazazi wao ni Umaskini uliokithiri pwani, ambapo watoto hawa wanaweza kupata lishe bora ikilinganishwa na majumbani mwao.
Si watoto walio na wazazi tu, bali pia watoto yatima wanatakikana kukuzwa katika jamii ili wao pia waweze kuwa na maadili ya kijamii.