Hali Ngumu Wakati wa Kufunguliwa Shule

By Khadija Mbesa

Malalamiko ya wazazi kuhusu hali ngumu ya maisha inayowapeleka wao kutoweza kuwapeleka wanafunzi shuleni. Bei ya juu ya vitabu vinavyotakikana shuleni, karo ya juu na ukosefu wa fedha wa mahitaji mengine yamekuwa vizuizi kwa wazazi hao kuweza kumudu mahitaji yote.

“Sina pesa ya kununua zaidi ya vitabu sita kwa mtoto wangu ambaye anajiunga na kidato cha kwanza katika shule moja ya hapa. Nikiwa na Sh3,000 tu, ninalazimika kuchagua vitabu vitatu kwa muhula wa kwanza, ”akisema mzazi mmoja katika pilka pilka ya kununua vitabu.

si hayo tu, bali wanafunzi wengine kukosa kurudi shule baada ya kupatwa na ujauzito ama kuolewa kwa sababu ya hali ngumu ya maisha ama kwa sababu ya mila. Hili likichongewa sana na hali ya janga la covid 19, ambapo wanafunzi wengi wamekuwa nyumbani.

Suala la kutokuwa na walimu wa kutosha limeleta tatizo pia, kwani walimu wanalazimika kuwasihi wazazi kuongeza kiasi cha karo ndipo waweze kumudu kuwaajiri walimu wengine.

Katika Kaunti ya Taita-Taveta, wazazi watalazimika kuchimba zaidi mifukoni mwao kufuatia kuletwa kwa ada ya ziada na shule zingine za sekondari za umma. wazazi pia watahitajika kulipia zaidi, maji, umeme, na wafanyikazi katika shule wanazosoma watoto wao.

“Tuna uhaba mkubwa wa walimu na tulikutana na wazazi kukubaliana juu ya jinsi ya kuajiri walimu zaidi. Nilikutana na wazazi wenye watoto katika kidato cha kwanza, cha pili, na cha tatu ambapo tulifanya azimio. Pia nitakutana na wazazi wa kidato cha nne na ikiwa hatukubaliani nao, basi nitaheshimu uamuzi wao,” Mkuu wa shule ya  Sekondari ya Canon Kituri, Bi Grace Mwawasi, alisema.

Siasa hizi zinawalazimu wazazi kukung’uta mifuko yao ili waweze kuwapeleka wanao shuleni.

source: https://www.standardmedia.co.ke/education/article/2001419236/parents-decry-tough-times-as-schools-reopen

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *