‘Hakuna Korti Itakayotoa Hukumu ya Kifo kwa Kosa Lolote Lililofanywa na Mtoto’

By Khadija Mbesa

Serikali ya Kenya,imetoa sheria mpya inayoelezea msururu wa faini kubwa kwa utelekezaji na unyanyasaji wa watoto, haswa katika maeneo ya mitandao ya kijamii na elektroniki.

Muswada wa Sheria ya Watoto, 2021, unataka kufuta Sheria ya Watoto, 2001, ili kuanzisha adhabu ya watakaomnyima mtoto haki ya kuishi, ustawi na maendeleo.

Muswada huo uliodhaminiwa na Kiongozi wa Wengi Amos Kimunya unapeana mamlaka ya serikali kuchukua hatua dhidi ya ukiukwaji wowote wa haki za watoto na kupuuzwa kwa uwajibikaji wa wazazi.

Wakati huo huo, sheria inayopendekezwa inataka kutoa kwamba “hakuna korti itakayotoa hukumu ya kifo kwa kosa lolote lililofanywa na mtoto.”

Pia ilipendekezwa kwamba, watoto wenye umri kati ya miaka 13 na 16 wanaweza kufanya kazi, chini ya sheria na masharti yaliyowekwa katika kanuni zilizochorwa na Katibu wa Baraza la Mawaziri la Kazi.

Sheria hii mpya pia inaruhusu mtoto mwenye umri wa miaka 12, na zaidi kufanywa kuwa sehemu ya kesi yoyote ya korti.

Watoto hawa, watakuwa na haki ya kugundua kesi, isipokuwa wakati korti itazingatia kutokuwa na faida kwa mtoto kuwa mshiriki kwenye kesi hiyo.”

Na la ziada ni kwamba, kila mtoto ambaye mzazi au mlezi wake hataweza kutoa msaada kwake, ana haki ya usalama wa kijamii kama inavyohakikishiwa na katiba.

Ikiwa wabunge wataidhinisha muswada huu, basi itakuwa kosa kwa mzazi kushindwa kuwapeleka watoto wao hospitalini, kwani watahatarisha faini ya Sh50,000 au siku 30 jela.

Sheria hii mpya, pia inaweka faini ya Sh2 milioni au miaka mitano gerezani, kwa tukio la kumnyanyasa mtoto kwa aina yoyote ya unyanyasaji, pamoja na shida ya kisaikolojia, kihemko na kiakili.

anazidi kuweka kifungo cha mwaka mmoja jela au faini ya Sh200,000 kwa tukio la kubagua mtoto kwa sababu ya umri, asili, jinsia, dini, imani, mila, lugha au hadhi, rangi, ulemavu, kabila, na makazi.

Watu ambao wananyima watoto urithi wao pia watawajibika kwa faini ya Sh500,000 au miaka miwili gerezani.

Sheria mpya pia inasema kwamba, mtu anayesababisha kifo cha mtoto, iwe moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja, kupitia mazoea mabaya atafungwa maisha.

Wazazi ambao huwapatia watoto wao dawa za kulevya kama vile pombe, tumbaku, dawa za kisaikolojia, au dawa yoyote mbaya, watakabiliwa na miaka mitano jela au faini ya Sh500,000.

Faini ya Sh2 milioni pia imependekezwa kwa mtu yeyote ambaye anapendekeza au kuomba kukutana na mtoto ili kushiriki katika vitendo vya ngono kinyume na Sheria ya Makosa ya Kijinsia.

Hizi ni sheria kadhaa katika katiba hii mpya kulingana na masuala ya watoto.

https://www.the-star.co.ke/news/2021-09-06-upkeep-for-children-born-out-of-wedlock-to-be-mandatory/

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *