Dawa za Mitishamba na COVID 19

By Martha Chimilila

Nchini Uganda,Mamlaka ya Kitaifa ya Dawa za Kulevya (NDA) imetoa onyo kwa wazazi na wakuu wa shule kuhusu matumizi ya dawa za mitishamba na Covidex kwa wanafunzi. Onyo hili limetolewa baada ya wadau kadhaa wa elimu kupinga wazo la wanafunzi kuripoti shuleni na dawa hizo kwa matumizi endapo watapata dalili za covid-19. 

Bwana Hasadu Kirabira, Mwenyekiti wa Chama cha Taasisi za Kitaifa za Elimu Binafsi alisema kuwa; 

”Kwa sasa nchi inafanya utaratibu na kutafuta njia salama ya kufungua tena, Taasisi za masomo ambazo tulifunga takribani mwaka na nusu.Ningependa kuwashauri Taasisi za elimu kuruhusu wanafunzi watumie dawa za mitishamba na covidex endapo watapata dalili za covid 19 wakiwa shuleni” 

Wazo hilo lilikataliwa wakati wa Mkutano wa Agosti 30 kati ya Wizara ya Elimu na wadau wengine wa elimu nchini Uganda. 

akitoa mfano wa wasiwasi wa utumiaji mbaya wa dawa na athari mbaya. 

Covidex iliidhinishwa na NDA kwa matumizi dhidi ya kupambana na maambuki ya virusi vya Covid 19, lakini wananchi wengi wa Uganda wamekuwa wakichukua  dawa hiyo hata wasipokuwa na dalili za ugonjwa. 

Bwana Abiaz Rwamwiri, Msemaji wa NDA, aliongea na waandhishi wa Daily Monitor tarehe 1 september na kusema kuwa; 

Covidex iliidhinishwa sio kama kinga (prophylaxis),ila inapaswa ufate ushauri wa mtaalamu wa afya kabla ya kuitumia. Kulazimisha watoto kununua wakati sio wagonjwa kunakuza utumiaji wa dawa zisizo salama. Tunawakumbusha umma kuwa dawa za kulevya hazipaswi kutumiwa kama vitafunio”  

Mamlaka ya kitaifa ya udhibiti wa dawa pia ilionya kwamba wanafunzi hawawezi kuwa na nafasi ya kuhifadhi salama dawa hiyo. 

“Pendekezo hili lina athari kubwa za usalama zinazohusiana na matumizi mabaya, uhifadhi duni na utumiaji wa dawa zisizosimamiwa. Dawa za kulevya ni nyeti kwa jinsi zinavyotunzwa na kutumiwa” 

Dk Misaki Wayengera, Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri wa Sayansi ya Covid-19 kwa Wizara ya Afya alisema kuwa; “Hakuna taarifa za kutosha kuunga mkono wazo la kuwapa watoto dawa hizo” 

Dk Kedrace Turyagyenda, Mkurugenzi wa Viwango katika Wizara ya Elimu alisema: 

“Kabla wizara ya Elimu haijatoa muongozo kwa wananchi wa Uganda,nawasihi tuache kusikiliza uvumi na habari mbaya dhidi ya Covid 19. Kila mtu ana haki ya kutoa mawazo yake lakini lazima yajadiliwe na kuthibitishwa kabla ya kutangazwa na kutengeneza mikakati” 

Source: https://www.monitor.co.ug/uganda/news/national/nda-warns-parents-against-using-covidex-for-children-3534994 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *