Daktari Aua Wanawe Wawili.

By Khadija Mbesa

Daktari anayedaiwa kuwaua watoto wake wawili kwa kuwadunga sindano ya dawa iliyopita kiasi, akamatwa hapo juzi katika kaunti ya Nakuru.

Mamlaka ilisema kwamba, daktari aliyetambuliwa kama Daktari James Gakara, alijaribu kujitoa Uhai kabla ya kukamatwa.

Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Nakuru, Beatrice Kiraguri, alisema kwamba, tukio hilo liliripotiwa na jirani katika eneo la Milimani mnamo saa tatu na nusu jioni Jumamosi.

Aliarifu kwamba, maafisa walikwenda na kuvunja nyumba ya Gakara, ambapo walimkuta daktari akiwa amelala bila fahamu katika chumba kimoja cha kulala, wakati watoto walikuwa wamekufa katika chumba tofauti.

Kiraguri alisema kuwa, dawa na sindano zilipatikana katika vyumba vyote viwili.

“Kulikuwa na kisu kilichonolewa katika chumba cha kulala cha watoto ambayo inamaanisha kuwa, daktari huyo alikuwa tayari kuwashtua au kuwakata koo ikiwa dawa hiyo itashindwa kufanya kazi,” akaongeza.

Miili ya watoto wawili wenye umri wa miaka 3 na 5, ilipelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Manispaa ya Nakuru, ikisubiri uchunguzi wa mwili kama sehemu ya uchunguzi.

Kiraguri alisema kwamba, mke wa daktari ambaye pia ni daktari alikuwa amesafiri kwenda Nairobi wakati kisa hicho kilitokea.

Daktari huyo, anamiliki Kliniki ya Huduma ya Afya ya Optimum ya sasa, katika Sehemu ya 58, mali ya Nakuru Town Mashariki.
Mkewe pia ni daktari na anafanya kazi katika kituo hicho hicho.

Alisema Gakara alikuwa katika hali nzuri katika Kitengo cha Huduma ya wagonjwa mahututi wa Hospitali Kuu ya Mkoa wa Bonde la Ufa.


“Amekamatwa na atakabiliwa na mashtaka atakapotoka hospitalini,” alisema Kiraguri.

Jirani alisema kwamba, wenzi hao wawili, hawakukubaliana Jumamosi alasiri wakati mama ya watoto hao, alisisitiza kusafiri nje ya nchi.

“Inaonekana kama mtu huyo hakupenda wazo hilo na akaamua kuua watoto na kuchukua maisha yake mwenyewe,” jirani alieleza.

Wakati kesi kama hiyo, ambapo daktari anaua watoto wake au watu walio karibu nae, ni nadra nchini Kenya, Swala la kujitoa uhai limekuwa likiongezeka mno, na wataalamu wanasema kwamba, swala hili linasababishwa na mafadhaiko, haswa kutokana na athari za kiuchumu za janga la COVID-19.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *