Covid Yazua Kadhaa

By Khadija Mbesa

Mtoto wa miezi sita aliyenyanyaswa kingono na babake wakati wa kufungiwa ndani kwa sababu ya maambukizi ya corona, Mtoto wa miaka kumi na nne ambae hakuweza kurudi shuleni wakati mzazi wake wa kiume,, mshirikii pekee wa kipato cha familia ametekwa na virusi hivi na kuaga dunia. Mtoto huyo huenda akalazimika kujitwika majukumu ya familia, na kuanza kutafuta kazi za mkono.

Kwa sasa kumekua na mawimbi mawili ya virusi vya covid 19, hata kabla ya watu kupumzika na kuuguza vidonda vya mbeleni, virusi hivi vimewapata vidonda vyao vikiwa bado vibichi.

Katika hali ya kupambana na njaa ili waweze kuishi, watoto hao wenye umri mdogo wanalazimika kuenda kufanya kazi za mkono mitaani ili waweze kupata vishillingi viwili ndio wamudu mahitaji ya familia, si hilo tu bali kuna muongezeko wa omba omba barabarani.

Ajira ya watoto hushinikiza mwisho wa masomo wa watoto hao, mathalan kwa kupata tonge la wali mkavu ni balaa, je wataweza kumudu fedha za sera ya shule?

Ndoa za mapema pia zimeongezeka kwa asilimia kubwa, watoto wa kike wanalazimika kuolewa ili waepuke shida zilizoko majumbani mwao baada ya walezi wao kuwa wahasiriwa na janga hilo la corona.

Ndoa za mapema zinaletwa baada ya watoto hao kukosa kwenda shule. Huu ni mduara ambao umeletwa na janga hili, na unawanyonya na kuwanyanyasa watoto zaidi.

Watoto hao wanaolazimika kulea watoto wenzao, kuwa wazazi utotoni, majukumu yanakuwa ngome yao. Vilio vyao ni minong’ono mbele ya serikali na Wanahisa.

Unyanyasaji wa watoto kingono, Ajira ya watoto na Ndoa za Mapema, Hili ni doa kubwa wakati tunazingatia Athari za Covid 19.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *