Chozi la Mama

By Khadija Mbesa

Kabla hatujaingia katika mjadala huu, tujitambulishe ni nini haswa afya ya kiakili?

Afya ya akili inahusu ustawi wa utambuzi, tabia, na hisia. Yote ni juu ya jinsi watu wanavyofikiria, kuhisi, na kuishi. Wakati mwingine watu hutumia neno “afya ya akili” kumaanisha kutokuwepo kwa shida ya akili.

Afya ya akili inaweza kukosesha ustawi wa Maisha na furaha ya Maisha. Kuwa na shida za kifedha ama kutengwa kwenye jamii inaweza kuwa mojawapo ya sababu zinazoleta maradhi hayo.

Kiasili Kuna ushahidi katika fasihi kwamba wazazi wa watoto walemavu hupata hatari kubwa ya shida za afya ya akili.

Utafiti huu ulitumia data ya kiwango cha idadi ya watu kutoka Wizara ya Afya, British Columbia, Canada, kutathmini afya ya akili ya wazazi wa watoto ambao wana ulemavu wa ukuaji ikilinganishwa na afya ya akili ya wazazi wa watoto ambao hawana ulemavu . Viwango vya idadi ya watu na vielelezo vya kibinafsi vinavyopatikana kwenye data vilijumuishwa katika modeli.

Utafiti huo uligundua kwamba kiwango cha idadi ya watu au wazazi wenye Watoto ambao wana ulemavu wa ukuaji wanapata hali mbaya ya unyogovu au utambuzi mwingine wa kiafya wa afya ya akili ikilinganishwa na wazazi wa Watoto ambao hawana ulemavu wa ukuaji.

Wazazi wa watoto ambao walemavu wanaweza kuhitaji mipango na huduma zinazosaidia afya yao ya akili.

afya ya akili ni sababu ya pili inayoongoza ya ulemavu. takwimu zinasema kwamba 1 kati ya 4 ana ugonjwa wa afya ya akili. mwanamke mmoja kati ya watano atapambana na afya ya wa akili wakati fulani katika maisha yake, na watu wengi hukaa kimya kwa sababu ya unyanyapaa.

Ishara za unyogovu ni tofauti kwa kila mtu, lakini zinapodumu kwa zaidi ya wiki nne na zinaingiliana na uwezo wetu wa kuendelea na maisha maisha, tuko katika nyakati za kuhitaji msaada kwa Maisha yetu.

Kila mzazi anaekuwa na ujauzito huwa anaswali na kuomba ya kwamba atapata mtoto salama wa salmini ila binadamu hupanga na Mungu pia anapanga, na wengine wao huweza kujifungua Watoto ambao wako na mapungufu ya kimaumbile ama shida za afya ya kiakili.

Hadithi fupi fupi kutoka kwa wazazi waliohasirika kwa sababu ya ulemavu wa Watoto wao, wazazi ambao wamejitwika gurudumu la ulezi peke yao kwani wengi wao wameachwa na mabwana zao.

Majirani kusema mtoto wako amelaaniwa, Watoto wengine hujitenga huku wakikataa kujumuika na mtoto, bwanako kutoroka majukumu yake kama mzazi kwa sababu hataki kujihusisha na mtoto huyo mlemavu. Je, ni masaibu mangapi wazazi wa kike wanao walea Watoto wenye ulemavu watapata?

Watoto wenye ulemavu ni moja ya vikundi vilivyotengwa katika jamii. Kukabiliwa na ubaguzi wa kila siku kwa njia ya mitazamo hasi, ukosefu wa sera na sheria za kutosha, wamezuiliwa kwa ufanisi kutimiza haki zao za utunzaji wa afya, elimu, na hata kuishi, kwa mfano maeneo ya Lamu kuna vikundi vya kijamii ambavyo haviruhusu wana wao walio na ulemavu kuenda shule.

Mara nyingi Watoto wananyimwa ufikiaji wa shughuli za kitamaduni, burudani au habari, na msaada kuhusu afya ya uzazi, ujinsia, na maeneo mengine ambayo ni muhimu kwa ujumuishaji wa mtoto kwa jamii na ukuaji wake hadi utu uzima.

Changamoto wanazokabiliana nazo watu wenye ulemavu ni nyingi mno na wazazi wao ndio ambao wanajizatiti kuwakuza.

Katika mwezi huu wa kuwakubali, kuwapatia moyo na kuwapa hongera wazazi wote ambao wanapitia shida za kifamilia, kuwa na upweke kwa sababu ya kutengwa, waliotupiwa maneno yasiyo mazuri wakiambiwa kua Watoto wao wana laana na mengineo.Si Wazazi tu bali pia Watoto walemavu wenye kupitia shida zizi hizi tunawapa moyo kuweza kuendelea kupigana na nafsi zao ili waweze kuibuka washindi katika vita hivi vya afya ya kiakili..

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *