By Khadija Mbesa
Pfizer kupanua vipimo vya chanjo ya Covid 19 kwa watoto walio na umri chini ya miaka kumi na miwili.
Kampuni ya pfizer ilisema kuwa itaanza kupima chanjo ya covid 19 katika kundi kubwa la watoto walio na umri chini ya miaka kumi na miwili baada ya kuchagua vipimo cha chini.
Kampuni ya Pharma ilisema, utafiti huo utasajili angalau watoto 4500 katika tovuti 90 na zaidi, za kliniki, Nchini Merika, Finland, Poland na Uhispania
Chanjo hiyo iliyotengezwa na Pfizer pamoja na Mshirima wake wa Ujerumani BioNTech, tayari imeruhusiwa kwa dharura kwa mtoto yeyote aliye na umri chini ya miaka 12 au zaidi, na wanapokea kipimo sawa na watu wazima ambayo ni mikrogramo 30.
Utafiti mpya wa Uandikishaji wa watoto wa miaka mitano hadi kumi na moja umeanza wiki hii. Pfizer ilisema kuwa, itajaribu kutumia kipimo cha mikrogramu kumi kwa watoto kati ya miaka mitano hadi kumi na moja na mikrogramu tatu kwa kikundi cha umri wa miezi sita hadi miaka mitano.
Msemaji wa Pfizer alisema kampuni hiyo inatarajia data maalum kutoka kwa watoto wa miaka 5-11 mnamo September na takwimu za watoto wa miaka 2-5 zinaweza kuwasili hivi karibuni.
Data ya watoto wa miezi sita hadi miaka miwili inatarajiwa mnamo mwezi Oktoba au November mwaka huu.