chanjo ya Covid 19 kwa wanaonyonyesha

By Martha Chimilila

Mama Wajawazito, Wanaonyonyesha Wahimizwa Kupata Chanjo ya Covid 19 (Uvido) 

Kituo cha Biomedical Rwanda (RBC) kimewahimiza wajawazito na wakina mama Wanaonyonyesha kwenda kupata Chanjo ya Uvido. Daktari Sabin Nsabimana, Mkurugenzi Mkuu wa RBC alisema yafuatayo: ‘Ninawahimiza wanawake wajawazito na watoa huduma za afya kuchomwa Chanjo’. Ujumbe huu umetolewa baada ya mlipuko wa janga jipya la kirusi Delta. 

Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) walitoa taarifa ya kuwa wajawazito wako kwenye hatari kubwa ya kupata ugonjwa huu, kulazwa na hata Uwezekano wa kufa kama hajapata Chanjo. 

Utafiti ulifanyika juu ya Ugonjwa wa Uzazi kati ya wanawake wajawazito wenye dalili za awali za Uvido. Tafiti zilionyesha kiwango cha chini cha kujifungua kwa njia ya Kawaida, na kiwango cha juu cha kujifungua kwa njia ya upasuaji na shida wakati wa kujifungua. 

Wataalamu kutoka Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa, walisema tafiti zinaonyesha kuwa, watu ambao walipata Chanjo za Uvido wakati wa ujauzito katika kipindi cha miezi mitatu ya mwanzo, wanaweza kupitisha kingamwili kwa watoto wao ambayo itawasaidia kuwalinda baada ya kuzaliwa. 

Daktari Sabin Nsabimana aliongeza kwa kusema kuwa “Chanjo haingiliani na mishipa ya damu ambayo mama na mtoto wanashirikiana” na “Tafiti zimethibitisha kuwa Chanjo haina athari haswa kwa wamama Wanaonyonyesha na watoto wachanga” 

Source: https://www.newtimes.co.rw/covid-19/pregnant-breastfeeding-mothers-encouraged-get-covid-vaccine 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *