By Martha Chimilila
Burundi ni moja ya nchi za Afrika Mashariki, ambazo zilipinga kufuata masharti yaliyotolewa na Shirika la Afya duniani juu ya janga la Uviko 19. Hali imekuwa ya tofauti baada ya serikali ya Burundi kuanzisha kampeni mbalimbali za kudhibiti na kukinga wananchi wake juu ya janga la Uviko 19. Katika juhudi za kuzuia kuenea kwa Uviko 19, Serikali ya Burundi mwanzoni mwa mwezi wa tisa, imeanzisha kampeni ya lazima ya utoaji wa chanjo kwa wanafunzi wote katika shule za bweni. Mpango huu utadumu hadi tarehe 14 Septemba,2021.
Moja ya vituo vya chanjo viko katika wilaya ya SOCARTIE, eneo la Kamenge, wilaya ya Ntahangwa kaskazini mwa Bujumbura. Wazazi na wanafunzi waliitikia kwa nguvu kampeni hii. Foleni ndefu zilianza kuundwa kuanzia mida ya saa nne asubuhi, na zaidi ya wanafunzi 400 walikuwa tayari wamechunguzwa wakati wa kurekodi ripoti hii.
Dk Thaddee Ndikumana, Waziri wa Afya ya Umma na Ukimwi nchini Burundi ulisema kuwa;
“Wanafunzi wamejibu kwa kiwango kikubwa. Tutafanya kazi kuwawezesha wanafunzi hawa kupata upimaji kwa urahisi na tumetoa wito kwa wale wanaosimamia tovuti kutoa upendeleo kwa wanafunzi,”
Kwenye tovuti hii ya uchunguzi kaskazini mwa Bujumbura, wazazi wengine waliandamana na watoto wao. Wengine walisema kwamba kampeni hii ni muhimu sana kuzuia kuenea kwa virusi shuleni.
“Mimi kama mzazi nakubaliana na hatua hii serikali iliyochukua ili kuwakinga watoto wetu. Kwa wazazi ambao bado hawajaelewa umuhimu wa chanjo nawaomba wajitokeze kwa wingi.”
Wanafunzi wanafahamu hatari ya ugonjwa huu na wengine wameelezea hofu yao juu ya uwezekano wa kukosa masomo, mmoja wa mwanafunzi aliyeenda kupatiwa chanjo alisema kuwa;
“Itaniathiri sana ikiwa nitapata dalili za ugonjwa wa Uviko 19. Huu ni wakati wa kujiandaa na mashindano ya Kitaifa napaswa kupata chanjo ili niweze kushiriki bila uwoga”