Athari za Muundo wa Familia kwa Watoto

By Khadija Mbesa

utafiti umetathmini athari za muundo wa familia kwenye afya na ustawi wa watoto kuwa, watoto wanaoishi na wazazi wao ambao wameoana au wazazi wa asili huwa na ustawi bora wa mwili, kihemko, na kielimu.

Je, talaka inaathiri vipi watoto?

Talaka sio mchakato rahisi kwa familia kupitia. Walakini, wakati mwingine talaka inakuwa sharti kwa wenzi hao, kwani wanaweza kuwa wamefikia njia panda katika ndoa yao, na yaweza kuwa bora kwa wote kutengana. Watu wazima wanaopitia mchakato wa talaka lazima wabadilike, na mabadiliko haya mapya ni pamoja na kuchukua maamuzi kadhaa yanayohusiana na hali ya kifedha na kihemko.

Utaratibu huu ni mgumu zaidi kwa watoto, haswa wakati wana umri mdogo, ambapo watoto hawawezi kuelewa mabadiliko mapya yanayotokana na ukweli wa kimsingi, kwamba hawataweza kuishi na wazazi wote kama familia moja. Kwa hivyo, watoto lazima wapate mabadiliko ya haraka ya kuishi na mzazi mmoja peke yake na kumuona mzazi mwenzake mara kwa mara tu, wakati wa ziara maalum. hii inasababisha mabadiliko ya kihemko na kutupilia mbali motisha ya mtoto kuishi na wazazi wote waawili.

Uchunguzi unaonyesha kuwa, mchakato wa talaka unaweza kuwa na athari zifuatazo kwa watoto, kulingana na umri wao:

Kwa watoto wachanga na watoto wa shule ya mapema : kwa sababu ni wadogo sana, watoto hawaelewi hitaji la kutengwa kabisa na mzazi mmoja. Dhana ya nyumba mbili zinaweza kujaza watoto wasiwasi na hofu. Wanahisi wasiwasi wakati hawawezi kuwa na wazazi wao wote na wanaweza kukaa kimya mara nyingi wakihisi kuwa, hawapendwi na mzazi aliyekuwepo.

Kwa watoto wa umri wa shule ya msingi : Mchakato wa talaka unaweza kuwasababishia mafadhaiko na wasiwasi, na mara nyingi huwafanya wahisi kuwa na hatia ju ya mabadiliko hayo, na kwamba talaka hiyo ni kwa sababu ya makosa au mapungufu yao.

Utafiti unaonyesha kuwa, watoto mara nyingi huathiriwa sana na talaka zenye ugomvi, ambazo zinaweza kudhihirika katika kuongezeka kwa shida za tabia, utendaji duni wa masomo na pia katika afya ya akili ya watoto.

Watoto wanahitaji kuzoea mabadiliko mapya, na moja wapo ya njia bora ni kufuata ratiba ya ziara ya kawaida na kuwapa ufikiaji rahisi kwa wazazi wote wanaokidhi mahitaji yao. Ratiba ya kawaida husaidia kuleta muundo unaozingatia mahitaji katika maisha yao, na watoto wanaweza kuelewa kuwa, wazazi wote hutanguliza mahitaji yao mara kwa mara. Msaada na uhakikisho wa wazazi unaweza kuzuia changamoto nyingi, haswa ikiwa wazazi wanaweza kutanguliza mahitaji ya watoto wao, kuliko kitu kingine chochote.

Wazazi wanapaswa pia, kuzingatia kutafuta msaada wa wataalam, ambao unaweza kujumuisha msaada wa matibabu ya kisaikolojia katika kuwasaidia watoto wao. Kutatua shida za wasiwasi kupitia msaada wa wataalamu, kumethibitisha kuwa ya thamani kubwa kwa watoto. Mtaalam mara nyingi anaweza kutambua sababu ya shida badala ya kuzingatia maswala ya tabia peke yake.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *