Athari za Maendeleo ya Kihemko ya kijamii

By Martha Chimilila.

Maendeleo ya kihemko ya kijamii yanahusisha uzoefu wa mtoto wa kujieleza na usimamizi wa mhemko na uwezo wa kuanzisha uhusiano mzuri na wenye tija kwa wengine. Ikiwa inahusisha michakato ya ndani na binafsi. Watoto wengi ambao wazazi wao walifanikiwa kukuza maendeleo ya kihemko na kihisia wameonekana wakifanya vizuri katika nyanja mbalimbali za Maisha. Vipengele vya msingi vya ukuaji wa kihemko ni pamoja na:

 “Uwezo wa kutambua na kuelewa hisia za mtu, kusoma kwa ufasaha na kuelewa hali za kihemko kwa wengine, kudhibiti hisia kali kwa njia ya kujenga, kudhibiti tabia ya mtu binafsi, kukuza uelewa kwa wengine, kuanzisha na kudumisha mahusiano”.

Vipengele hivi vya ukuaji vinawasaidia katika hali ya utu uzima kwa kuwa na uwezo wa Kujadili mwingiliano wa kijamii, Kushiriki vyema katika mahusiano na shughuli mbalimbali katika maendeleo na utendaji kazi mzuri wa Kibinadamu. Lakini tafiti zinaonesha kuwa hisia na utambuzi ni michakato zinazohusiana kutoka hatua ya utoto hadi utu uzima, katika kutoa maamuzi, kujifunza na kuomba msaada pale inapohitajika.

Njia za kukuza maendeleo ya kihemko kwa Watoto:

Kua muhimili wao wanapopata matatizo na kuwatia Imani ya kua wanaweza kufanya jambo lolote, hii inawapa hali ya kujiamini katika kutoa maamuzi, kufanya kazi, kielimu na pia hata kusimamia mambo ya kijamii, kiuchumi na kifamilia.

Pia Yatengeza ratiba ya michezo kati yako na watoto, hakikisha kila wiki unapata wasaa wa kukaa, kupata mlo wa pamoja na kuwapatia nasaha za kimaisha.

Kuwaonesha upendo na hisia zako kwa kuwakumbatia, kuwabusu, kuwasikiliza, kuwajali hata kwa vitu vidogo vidogo na kuwauliza maswala muhimu kuhusu Maisha yao ya kila siku. Mzazi anapaswa kutengeneza ukaribu na Watoto katika kipindi chote cha ukuaji ili waweze kufahamu umuhimu wao katika jamii, binafsi na familia. Huu ukaribu utaleta uwezo wa mtoto kutengeneza mahusiano yenye tija na pia kuweza kuelewa mwenza wao katika kipindi cha utu uzima.

Kuwatia moyo na kuwashawishi kufanya jambo jipya kila mara na hata lisipoleta matokeo chanya, waoneshe kua unapendezwa na kila hatua wanayopitia. Wape fursa ya kucheza na Watoto wengine, wasaidie katika tafiti zao za kutambua wao ni nani na wapi wangependa kufika katika maisha yao ya baada.

Athari Hasi za Maendeleo ya Kihemko:

Dunia imepata kuona visa vingi vya ukatili wa kijinsia, unaotokana na kutotengeneza mipango madhubuti ya kukuza mhemko na hisia za Watoto wangali ni wadogo.

Tafiti zinaonesha kuna ongezeko kubwa wa uvunjikaji wa ndoa ni, Kushindwa kufahamu hisia za mwenza wake na kuleta matatizo makubwa hata kwa kizazi kingine.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *