Ajira ya Watoto na Utumwa Kuongezeka

By Khadija Mbesa

Watoto wana hatari zaidi ya kusukumwa katika ajira ya watoto kama matokeo ya Covid-19, ambayo inaweza kusababisha kuongezeka kwa utumikishwaji wa watoto, baada ya miaka 20 ya maendeleo.

Shirika la wafanyikazi ulimwenguni linaonya kuwa, visa vingi vya ajira na utumwa vinaripotiwa katika uchumi wa Kusini mwa Jangwa la Sahara na Asia, na nchi kadhaa zikiwemo Kenya. 

 Kumekuwa na ongezeko la vijana na watu wazima haswa wanawake wanaotoka Kenya, Uganda, Eritrea na Ethiopia kwenda nchi za Ghuba tangu janga hilo lilipotokea duniani, ” inasema sehemu ya ripoti hiyo. 

Hii inahusishwa na kufungwa kwa shule kama hatua ya kuzuia kuenea kwa Covid-19, mnamo 2020 na kiwango cha juu cha umasikini katika nchi hizo. 

Mashirika mengi yameripoti kuongezeka kwa ajira kwa watoto, baada ya kuzuka kwa janga hilo.

Kulingana na utafiti uliofanywa na Mtandao wa Kiafrika, wa Kinga dhidi ya Unyanyasaji na Utelekezaji wa Watoto (ANPPCAN), katika kaunti nne nchini Kenya, watoto wengi waliathiriwa wakati shule zilifungwa kwa sababu wazazi wengi huko, walikuwa wamejiajiri katika Sekta isiyo rasmi, wakiwa wakulima wa muda mfupi wakizalisha kipato kidogo.

Makadirio ya ulimwengu mnamo 2017 yalionyesha kuwa, watoto milioni 152 walikuwa katika ajira ya watoto ulimwenguni.

Covid-19 inaweza kusababisha kuongezeka kwa umaskini, na kwa hivyo kuongezeka kwa ajira ya watoto kwani kaya hutumia kila njia inayopatikana kuishi.

Baadhi ya tafiti zinaonyesha kuwa, ongezeko la asilimia moja la umasikini husababisha angalau ongezeko la asilimia 0.7 ya ajira kwa watoto katika nchi fulani.  

Janga la Covid-19 limeosababisha maelfu ya wazazi kuachishwa kazi kutoka kwa bara zima huku likisukuma familia nyingi kwa umasikini uliokithiri.

Nchini Kenya pekee, katika miezi mitatu tu ya kwanza ya janga hilo, Ofisi ya Takwimu ya Kenya ilitangaza kwamba zaidi ya Wakenya milioni 1.7 wamepoteza kazi.

https://www.the-star.co.ke/business/kenya/2021-08-25-child-labour-and-slavery-surge-on-covid-19-ilo/

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *