Afya ya Watoto na Mitandao ya Kijamii

By: Martha Chimilila

Mitandao ni nyenzo ya msingi ya maendeleo katika nyanja ya Mawasiliano, ambapo jamii mbalimbali ulimwenguni wanaunganishwa. Matumizi ya simu za mikononi na zana mbalimbali za kidigitali, zimeongezeka sana katika kipindi hiki ambacho dunia inapambana na janga la Corona. Kutoka mwaka wa 2019 na kuendelea tumeona kuwa, idadi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii na tovuti wameongezeka, hii ni kufuatia Mabadiliko ya teknolojia, uhitaji wa taarifa, na ununuzi wa vitu mbalimbali katika Maisha ya kila siku.

Tafiti zaonesha kuwa, kuna ongezeko la watumiaji wa mitandao na Watoto wakiwa miongoni mwao, ambapo zaidi ya asilimia 60 ya Watoto duniani wanaweza kutumia mitandao ya simu bila ya idhini au usimamizi wa wazazi. “Dr Herzon Zakaria wa chuo Kikuu cha Dar es Salaam” alifanya utafiti juu ya unyanyasaji wa mitandao kwa Watoto nchini Tanzania. Watoto wamekua wakipokea Maoni mabaya hususan maoni kuhusu miili yao, huku wakikumbana na lugha za matusi, unyanyasaji wa kingono, kuchekwa maumbile yao pamoja na vitisho vya unyanyasaji wa kijinsia, ambayo inaleta athari za afya ya akili.

Aliweza kubaini kwamba, watoto wengi wameathirika kisaikolojia kutokana na kuwekwa kwa mitandao kama njia ya kupata umaarufu. Mtoto wa muigizaji maarufu nchini Tanzania, alitoa maelezo yafuatayo:

Mimi ni mtoto ambaye nina marafiki zaidi ya 500 ambao siwafahamu hata nikipokea Maoni au ujumbe mfupi inakua ni vigumu sana kusema ninachofanyiwa hivyo unakuta nakaa kimya na kuumia moyoni na tusipopata msaada au watu wakutusikiliza unakuta tunaathirika kisaikolojia, mahusiano na marafiki au wana familia au ndugu, tunaathirika kitaaluma na kushindwa kuwa makini katika kusoma na kujifunza

Tafiti zaonesha takribani asilimia 42 ya Watoto ambao ni sawa na Watoto wanne kati ya kumi wamewahi kunyanyaswa mitandaoni. Tatizo hili si la Tanzania pekee ila dunia nzima, Watoto wanatumika kama njia ya kuwaadhibu wazazi kwa makosa ambayo wanafanya kwa jamii.

Mfano mwingine wa ukatili wa kijinsia mitandao ni:

” Upigwaji wa picha na kusambaza mitandaoni; hii ni hali ambayo watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu wanapigwa picha ili wapate misaada. Jambo ambalo ni ukiukwaji wa haki za Kibinadamu na haki za watoto. Hili husababisha madhara makubwa wakati wa utu uzima

Kutokana na ongezeko la ukatili dhidi ya watoto katika nchi mbalimbali duniani. Tanzania, ikishirikiana na Mashirika zaidi ya 40 yalikutana kutafuta mbinu za kukomesha udhalilishaji wa watoto kwenye mitandao ya kijamii.

Nini kifanyike ili kuondoa tatizo hili?

Utoaji wa elimu dhidi ya ukatili wa kijinsia mitandaoni ambao una athari sawa sawa na ukatili wa aina yeyote ya kijinsia. Wanaofanya vitendo vya unyanyasaji mitandaoni, wanafanya kwa kutokua na uelewa au kwa makusudi kutokana na Maisha ambayo wamepitia.

Kutengeneza sheria shirikishi ambazo zitamlinda mtoto kutokana na vyombo vya habari na mitandao. Kwa mfano, tunashuhudia matumizi ya video au picha za mnato zikisambaa mitandaoni. Wazazi pia wanastahili kudhibiti matumizi ya mitandao ya kijamii kwa Watoto. Ushirikiano kati ya serikali hasa vyombo vya kisheria pamoja na kuunda madawati ya kijinsia na, Asasi zinazoshughulikia haki za Watoto na wadau mbalimbali wa maendeleo ya Watoto duniani.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *